Masharti ya Matumizi

Terms & Conditions – VicobaPlus

Tafadhali soma masharti haya kwa makini kabla ya kutumia mfumo wa VicobaPlus. Kwa kutumia mfumo huu, unakubali masharti yaliyoainishwa hapa chini.

1. Kuhusu Mfumo

VicobaPlus ni mfumo wa kidigitali unaotolewa na Fayam Technologies Ltd kwa ajili ya kusaidia vikundi vya Vicoba kusimamia wanachama, hisa, mikopo, marejesho, mapato, matumizi na ripoti.

2. Usajili wa Kikundi

Ili kutumia mfumo, kikundi kinatakiwa kujisajili kwa kutoa taarifa sahihi. Mtumiaji anawajibika kuhakikisha taarifa zote zilizowekwa ni sahihi na halali.

3. Malipo ya Huduma

Matumizi ya mfumo yanahitaji malipo kulingana na mpango uliopo. Kikundi kinapaswa kulipa kwa wakati ili kuendelea kutumia huduma.

Kushindwa kulipa kunaweza kusababisha kusimamishwa kwa huduma hadi malipo yatakapokamilika.

4. Usalama wa Taarifa

Tunajitahidi kulinda taarifa za watumiaji kwa kiwango cha juu. Hata hivyo, kikundi kinapaswa kuhakikisha akaunti zao zinalindwa kwa kutunza nenosiri kwa usalama.

5. Matumizi Sahihi ya Mfumo

Mfumo huu hautakiwi kutumika kwa shughuli zisizo halali au kinyume na sheria. Fayam Technologies ina haki ya kusimamisha huduma endapo matumizi mabaya yatabainika.

6. Uwepo wa Mfumo

Tunajitahidi kuhakikisha mfumo unapatikana muda wote. Hata hivyo, kunaweza kutokea matengenezo au hitilafu za muda mfupi zisizotarajiwa.

7. Mabadiliko ya Masharti

Fayam Technologies Ltd ina haki ya kubadilisha masharti haya wakati wowote. Mabadiliko yatatangazwa kupitia mfumo au njia rasmi za mawasiliano.

8. Mawasiliano

Kwa maswali au msaada, tafadhali wasiliana nasi kupitia:

  • Simu: 0766574792
  • WhatsApp: 0718337728
  • Email: info@shariavicoba.com